Alhamisi 12 Februari 2026 - 14:46
Wanazuoni wa Kiislamu na wasomi ulimwenguni watoa wito wa kuitikia kauli ya Kiongozi wa Waislamu duniani

Hawza/ Baadhi ya shakhsia mashuhuri za kielimu na kifikra katika ulimwengu wa Kiislamu, wakijibu kauli ya Kiongozi wa Mapinduzi, kwa kutuma ujumbe wa pamoja wa video, wameitaja tarehe 22 Bahman kuwa ni nukta ya mageuzi katika historia ya mwamko wa Kiislamu na alama ya kusimama imara dhidi ya ubeberu wa kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanazuoni, wanafikra na wasomi katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuitikia kauli ya Walii wa Amri wa Waislamu duniani, kupitia uchapishaji wa video mbalimbali, walisisitiza umuhimu na nafasi ya kimkakati ya 22 Bahman ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ujumbe huo imeelezwa wazi kwamba 22 Bahman si mali ya taifa la Iran pekee, bali ni siku ya kihistoria na yenye kutia hamasa  Umma wote wa Kiislamu. Kwa mtazamo wao, 22 Bahman ni alama ya kusimama imara, azma na ustahimilivu wa Umma wa Kiislamu mbele ya mkondo wa ubeberu wa kimataifa.

Walisema kuwa; Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya tarehe 22 Bahman yana funzo kubwa kwa Umma wa Kiislamu na watu wote huru duniani; funzo linaloonesha kwamba ni kwa kusimama imara na kwa mapambano ya upinzani pekee ndipo utambulisho halisi wa Kiislamu, heshima na kuinuka kwa Uislamu mtukufu vinaweza kuhifadhiwa na kulindwa katika dunia ya leo iliyojaa uchafu na utawala wa mabavu, na pia kuwasilishwa kwa walimwengu.

Wanazuoni na wasomi hawa waliyataja Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mfano hai wa mapambano ya upinzani yaliyofanikiwa, na wakaitambulisha 22 Bahman kuwa ni nukta ya mageuzi katika historia ya mwamko wa Kiislamu na yenye kuhamasisha harakati za kupigania uhuru katika ulimwengu wa Kiislamu.

Majina ya wanazuoni hao:

1- Sheikh Khalid al-Mulla, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlus-Sunna wa Iraq

2- Sheikh Ghazi Hanina, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon

3- Sheikh Hussein Qasim, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Palestina

4- Sayyid Adnan al-Junaid, Kiongozi wa Tasawwuf wa Yemen

5- Sheikh Hassan al-Baghdadi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah Lebanon

6- Maulawi Habibullah Hussam, Mkuu wa Baraza la Udugu wa Kiislamu Afghanistan

7- Sheikh Bilal Shaaban, Mkuu wa Harakati ya Tawhid ya Kiislamu Lebanon

8- Sheikh Talal Abdulrahman, mfungwa huru wa Palestina na msimamizi wa faili la wafungwa wa Palestina ndani ya Hamas

9- Sheikh Yusuf Mashlawi, Mkuu wa Tayar al-Muqawim Palestina

10- Dkt. Yahya Abu Zakaria, mchambuzi mwandamizi wa kimataifa kutoka Algeria

11- Bi. Alia al-Yasir, mwanahabari na mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Iraq

12- Sheikh Sayyid Bahauddin Naqshbandi, murshid wa Tariqa Naqshbandiyya Kurdistan ya Iran na Iraq

13- Sheikh Abdullah al-Daqqaq, Mkurugenzi wa Hawza ya Wabahrain

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha